CCM LEADERS

CCM


I made this at .

Wednesday, 29 September 2010

New Generation -Labour Party Conference


Thursday, 16 September 2010

Mkutano wa Kampeni Arusha Mjini: JK aitikisa Arusha!
Julius Msekwa Afariki DuniaMAREHEMU JULIUS MSEKWA.
----

FAMILIA YA PIUS MSEKWA INA HUZUNI KUTANGAZA KIFO CHA MPENDWA WAO JULIUS MSEKWA, KILICHOTOKEA PARALIMNI, CYPRUS, JUMAMOSI YA TAREHE 11/09/2010.

JULIUS ALIKUWA AKIISHI NA KUFANYA KAZI NCHINI UINGEREZA TANGU MWAKA 1996, ALIKUWA AMEKWENDA CYPRUS KWA MUDA MFUPI ,AMBAPO NDIKO MAUTI YALIPOMFIKA.TARATIBU ZA KUREJESHA MWILI DAR ES SALAAM KWA AJILI YA MAZISHI ZIMEKAMILIKA NA MWILI WA MAREHEMU UNATARAJIWA KUWASILI JUMAPILI 19/09/2010, ALFAJIRI KWA NDEGE YA EGYPT AIR.

MAZISHI YATAFANYIKA JUMATATU 20/09/2010 KATIKA MAKABURI YA KINONDONI, DAR ES SALAAM.MSIBA UPO NYUMBANI KWA NDUGU PIUS MSEKWA, NO. 13 BONGOYO RD. OYSTERBAY.

KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU, SALA ZETU WOTE NI KUMUOMBA MWENYEZI MUNGU AIWEKE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI.

Thursday, 9 September 2010

Kampeni katika picha Kilindi, Handeni

Shamra Shamra zamsubiri JK Handeni


Tuesday, 7 September 2010

Twanga Wapepeta Na Amos Makalla Mvomero
JK akimnadi mgombea ubunge wa CCM jimbo la Mvomero, Morogoro, Mh. Amos Makalla katika uwanja wa michezo wa Mvomero Jumapili
JK akiongea na wananchi kibao waliokuwa wametanda njia nzima wakati akielekea Mvomero.

Wadau wa Mtibwa Sugar wakiwa katika mkutano wa kampeni wa JK Mvomero
Wadau wa CCM toka Dar walikuwepo kumpa tafu Amos Makalla
Twanga wakipepeta Mvomero Jumapili
wadau wa Twanga Pepeta wakisikiliza hotuba ya JK mvomero
Toka shoto ni Rogert Hegga 'Katapila', Hamisi Amigoras na Lwiza Mbuttu
Ben Kinyaiya (shoto) akiwa na wana Twanga Pepeta
Abuu Semhando 'Baba Diana' akiwa na Omari Baraka Mvomero

Monday, 6 September 2010


Picture

Saturday, 4 September 2010

Jamhuri Stadium Yafurika - Mkutano wa Kampeni Morogoro Mjini

Pikipiki ikiongoza kumsindikiza Mgombea wa CCM Mheshimiwa Kikwete wakati msafara wake ukiingia Morogoro mjini.
Mgombea Urais wa CCM Mheshimiwa Kikwete akimnadi mgombea Ubunge wa CCM Morogoro mjini Aboud kwenye uwanja wa Jamhuri leo.

Mheshimiwa Kikwete akihutubia umati wa watu uliofika Jamhuri Stadium jioni ya leo kuhudhuria Mkutano wa kampeni.
Friday, 3 September 2010

JK Azungumza Na Viongozi Wa CCM Kawe Na Ubungo
1. Mwenyekiti wa CCM Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia baadhi ya wanachama wa CCM muda mfupi baada ya mkutano na viongozi wa CCM jimbo la Kawe jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
2. Mwenyekiti wa CCM Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na viongozi wa CCM wa Ubungo na Kinondoni katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam leo mchana.

3. Baadhi ya wanachama wa CCM wakimsikiliza Mwenyekiti wa CCM Dr.Jakaya Mrisho Kikwete katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam leo mchana(Picha: Freddy Maro)

Kibao Kipya cha Kampeni za CCM -Vuvuzela

Thursday, 2 September 2010

Kampeni Ya Mgombea Urais Wa CCM Jakaya Mrisho Kikwete Tukuyu
Mgombea Urais wa CCM Jakaya Mrisho Kikwete akisalimia na wana Tukuyu akipo Richard Kasesela ambaye aligombea ubunge jimbo la Rungwe Magharibi na kubwagwa na Prof. David Mwakyusa.

Wednesday, 1 September 2010

.Mkutano wa Kampeni Mbeya Mjini: JK anasimikwa na Wazee wa Mbeya, akabidhiwa vifaa Vya Kazi

Tuesday, 31 August 2010

Wananchi Msistuke Pindi Muonapo Ndege Na Helikopta Za Kivita
Mkuu wa Majeshi nchini Jenerali Devis Mwamunyange
-------------
Benjamin Sawe-Maelezo,Dar es Salaam.


Wakazi wa Dar es Salaam hususani Kigamboni wametakiwa kutoshtuka mara waonapo ndege pamoja na helikopta ya kivita zikipita maeneo ya anga la Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Sadiki imesema kuwa wananchi wanatakiwa kutokuwa na hofu yoyote kwani hiyo ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Majeshi.

Taarifa hiyo imeongezea kuwa pamoja na mambo mengine hapo kesho tarehe 1/9/2010 watarusha ndege za kivita pamoja na helikopta.

Katika maadhimisho ya wiki ya majeshi mgeni rasmi katika ufunguzi atakuwa Mkuu wa Majeshi nchini Jenerali Devis Mwamunyange na tarehe 1/9/2010 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Daktari Hussein Ali Mwinyi atakuwa mgeni rasmi.Kila mwaka JWTZ huadhimisha Wiki ya Majeshi ambapo kwa kawaida inaanza tarehe 26/8/2010 hadi tarehe 1/9/2010.

Mkutano wa Kampeni Mbeya Mjini: JK anasimikwa na Wazee wa Mbeya, akabidhiwa vifaa Vya Kazi

Chifu Mkuu wa Mbeya Chifu Mweshenga na machifu wengine wa wilaya zote Mkoani Mbeya wamemsimika Mheshimiwa Jakaya Kikwete ikiwa ni ishara ya kumkaribisha Mkoa wa Mbeya na alama ya uongozi.


Wakimsimika rasmi kama kiongozi, machifu hao wamesema ujio wa wana CCM na wananchi wengi Mkoani Mbeya ni ishara nzuri ya ushindi wa kishindo kwa CCM na Mheshimiwa Kikwete.

Chifu Mweshenga ameanza kwa kumvika shuka nyeupe ishara ya uongozi wa ki-chifu kwa mkoa wa Mbeya. Pia Chifu huyo amemkabidhi Mheshimiwa Kikwete Mkuki na kusema "Mheshimiwa wewe ni kiongozi sasa lakini pia ni mwanaume (hivyo kwa mila yetu) unatakiwa kuwa na mkuki ndani ya nyumba"

Mwisho kabisa machifu hao wa Mkoa wa Mbeya walimkabidhi Mheshimiwa Kikwete kiti cha jadi na kusema kwamba wao wanaamini kuwa mgombea huyu wa CCM atarudi Ikulu, na hivyo atumie kiti hicho kukalia na kufanya maamuzi muhimu ya uongozi.

Ujumbe huu wa Machifu uliongozwa na Chifu Mkuu Mkoani Mbeya Chifu Mweshenga, Katibu wa Machifu Mkoa Chifu Mwaluego, Chifu Kiongozi Mkoa Chifu Lioto, Chifu Mwongole na Chifu Richard Mwavipa.

Saturday, 28 August 2010

JK Awasili Mpanda
Mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akimsalimia mtoto ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja muda mfupi baada ya mgombea huyo kuwasili katika uwanja wa michezo wa mjini Mpanda ambapo alihutubia wananchi katika mkutano wa kampeni jana mchana.Baadhi ya wakazi wa mji wa Mpanda wakimkaribisha kwa mabango mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, Dr.Jakaya Mrisho Kikwete jana mchana.


Friday, 27 August 2010

Mama Salma Kikwete Akiwa Wilayani Mafia

Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete akimtambulisha mgombea ubunge wa Mafia kupitia CCM,Bw. Abdulkarim Shah.
Mwenyekiti wa Taasisi ya wanawake na Maendeleo (WAMA) ,Mama Salma Kikwete,akiongea na wanachama wa UWT Wilaya ya Mafia katika ziara ya siku moja kuwahamasisha wanachama wa umoja wa wanawake Tanzania kuwachagua wagombea wa CCM katika uchaguzi ujao.
Wanachama wa UWT Wilayani Mafia Mkoa wa Pwani wakimsikiliza Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete hayupo pichani katika mkutano wake na wanachama hao kuhusu kuwahamasisha masuala ya Uchaguzi Mkuu ujao hapo Oktoka 31 mwaka huu.
(picha zote na Mwanakombo Jumaa-Globu ya Jamii)

Jakaya Kikwete awasili Kigoma
JK akipungia mkono baada ya kutua kijijini
Buhingwe, Kigoma vijijini, kwa helikopta akitokea Ngara na kuelekea Uvinza
JK akimnadi mgombea ubunge wa CCM wa
Kigoma mjini Peter Serukamba mjini Kigoma

Kinamama wakimshangilia JK alipohutubia umati
mkubwa wa wananchi wa Kigoma mjini

JK alipokuwa Karagwe
JK akihutubia Kigoma mjini

DR. Bilal aendele kuinadi ilani ya CCM mkoani mtwara
Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. Mohamed Gharib Bilal akimnadi mgombea ubunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe baada ya kuingia Wilayani Nachingwea.
Wananchi wa Nachingwa wakimsikiliza Mgombea Mwenza wa nafasi ya urais Dk. Mohamed Gharib Bilal alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Wilaya ya Nachingwea katika uwanja wa Sokoine leo mchana
Mgombea Mwenza wa urais ,Dk. Gharib Bilal akiongozana na Mgobea Ubunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe baada ya kupokelewa mpakani mwa Wilaya ya Liwale na Nachingwea wakati wa zaiara yake ya kunadi ilani ya Chama cha Mapinduzi katika kampeni za kukiombea kura Chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao unaotarajia kufanyika Oktoba 31 mwaka huu.
Mohamed Gharib Bilal, akipokelewa na Diwani wa Viti maalum, Asina Lutumbo na Mwenyekiti mstaafu wa UWT, Anna Abdalah, baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Sokoine wilayani Nachingwea alipofika kufanya mkutano wa kampeni leo

kwa picha zaidi

BOFYA HAPA

JK ndani ya kijiji cha Rusahunga

Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akimsalimia na kumsikiliza msichana mlemavu Joyceline Paulo huko Rusahunga wakati mgombea huyo aliposimama kuwasalimia wananchi na kunadi ilani ya CCM.Dr.Kikwete aliahidi kumpatia mlemavu huyo baiskeli maalumu ya matairi matatu ili aweze kumudu shughuli zake kwa urahisi zaidi.Dr. alikuwa njiani akitokea Ngara mkoani Kagera kuelekea Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kwa barabara
Dr.Kikwete akiwahutubia wananchi wa kijijini Rusahunga wakati aliposimama kuwasalimia na kunadi ilani ya CCM wakati alikuwa njiani akitokea Ngara mkoani Kagera kuelekea Wilayani Kibondo mkoani Kigoma kwa barabara.
(Picha na Freddy Maro)

JK Na Watoto

Mwanafunzi Joel Abdallah anayesoma darasa la tatu katika shule ya msingi Rutozo iliyoko katika kijiji cha Katoro wilayani na mkoani Geita, akimsalimiana na Rais Kikwete wakati akiwa katika kampeni za kuwania urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) hivi karibuni.

Thursday, 26 August 2010

Nkuruzinza Aapishwa
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimpongeza Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza baada ya kuapishwa kuwa rais wan chi hiyo Mjini Bujumbura Augosti 26, 2010. Katikati ni mke wa rais huyo,Deruse Nkurunzina.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Mkutano wa Kampeni – Rulenga: JK Akabidhiwa Silaha za Jadi

Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amekabidhiwa silaha za jadi na wananchi wa Rulenga ili aweze kujiandaaa vizuri cha uchaguzi.

Silaha hizo ni shoka la kufyekea visiki njiani anapopita kusaka kura za wananchi, panga kujilinda na hatari zilizombele yake na kusafisha njia na mwisho ni mkuki ambao ni ishara ya ushindi na uongozi. Wana Rulenga wameahidi kumpa kura zao zote za ndio Mgombea wa CCM Mheshimiwa Kikwete na wanaimanii atashinda kama kiongozi wa nchii na hivyo wamempa silaha hizo kama kiongozi.

Rulenga ambayo iko ndani ya Wilaya ya Ngara ni kituo cha pili baada ya Ngara Mjini ambapo msafara wa Mgombea Urais CCM ambapo kulikuwa na wananchi wengi na vikundi mbalimbali vya ngoma vikimsubiri.

Kabla ya kuanza hotuba yake, Mheshimiwa Kikwete alikosha nyoyo za wana Rulenga kwa kucheza wimbo wa pipi remix CCM Version ya mwanamziki wa kizazi kipya Marlow. Staili hii ya mgombea imekonga nyoyo za wana ccm wengi kote alikopita kwa staili yake ya uchezaji ambapo kundi la Vijana Zaidi wameipa staili hiyo jina la JK shafo (shuffle)

Baada ya Rulenga Mheshimiwa Kikwete alisimama Lusahunga kusalimia wananchi na baadae alielekea Biharamulo kwenye Mkutano wake wa tatu wa Kampeni kwa siku ya leo.

Kutoka Press Kikwete 2010
JK: No going back on anti-graft fight

Monday, 23 August 2010

Picha Za Hafla Ya Kumwaaga Aliyekuwa Katibu Wa Shina La CCM Reading Mh.Benjamini M Maira
Sunday, 22 August 2010

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, Taifa, Rais Jakaya Kikwete akipungia maelfu ya wana CCM, muda mfupi kabla ya kuzindua rasmi kampeni ya chama hicho Jangwani Jijini Dar es Salaam jana.(Picha: Selemani Mpochi).

Kikwete: Nitashinda kwa kishindo

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, Rais Jakaya, Kikwete, jana alizindua rasmi kampeni za chama hicho kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani, utakaofanyika Oktoba mwaka huu, na kujigamba kuwa ataibuka na ushindi wa kishindo kwani ametimiza ahadi nyingi alizowaahidi wananchi wakati wa uchaguzi mkuu uliopita Habari Kamili

Older Posts