CCM LEADERS

CCM


I made this at .

Tuesday 31 August 2010

Wananchi Msistuke Pindi Muonapo Ndege Na Helikopta Za Kivita
Mkuu wa Majeshi nchini Jenerali Devis Mwamunyange
-------------
Benjamin Sawe-Maelezo,Dar es Salaam.


Wakazi wa Dar es Salaam hususani Kigamboni wametakiwa kutoshtuka mara waonapo ndege pamoja na helikopta ya kivita zikipita maeneo ya anga la Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Sadiki imesema kuwa wananchi wanatakiwa kutokuwa na hofu yoyote kwani hiyo ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Majeshi.

Taarifa hiyo imeongezea kuwa pamoja na mambo mengine hapo kesho tarehe 1/9/2010 watarusha ndege za kivita pamoja na helikopta.

Katika maadhimisho ya wiki ya majeshi mgeni rasmi katika ufunguzi atakuwa Mkuu wa Majeshi nchini Jenerali Devis Mwamunyange na tarehe 1/9/2010 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Daktari Hussein Ali Mwinyi atakuwa mgeni rasmi.Kila mwaka JWTZ huadhimisha Wiki ya Majeshi ambapo kwa kawaida inaanza tarehe 26/8/2010 hadi tarehe 1/9/2010.

0 comments:

Newer Post Older Post Home